... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Matata ya Kutosha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 8:11-13 Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu. Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo.

Listen to the radio broadcast of

Matata ya Kutosha


Download audio file

Ikiwa uko kama mimi, utapenda maisha yako yaratibishwe vizuri bila matata.  Nadhani sisi sote tuna matumaini kwamba maisha yataeleweka, kwamba watu watakuwa na mtazamo kama sisi na kutuitikia kama tunavyotazamia sisi.  Lakini, itawezekana kweli!?

Tunajua kwamba maisha hayaendi kama tunavyopanga sisi wala kama tunavyofikiri. Angalia mfano wa Yesu. Popote alienda alitenda mema tu.  Aliwaponya wenye ukoma, vipofu na wenye magonjwa sugu. Alionyesha neema ya Mungu kwa wenye dhambi na waliotengwa na jamii.  Mahubiri yake yalikuwa na nguvu akitumia mifano ya maisha ya kila siku, mifano iliyoeleweka vizuri na kutikisa kabisa watu wa kawaida.  Lakini hata hivyo, viongozi wa dini hawakuridhika. 

Mariko 8:11-13  Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu.  Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara?  Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.  Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo. 

Jamani! Hawakuona wazi yale mema yote aliyokuwa anatenda?  Kwanini hawakuguswa wakimshangaa kama wengine wote?  Lakini … hivi ndivyo vilivyomgharimia. 

Msanii, akiwa pia mwandishi na mchungaji aitwaye Mandy Smith aliandika hivi:  Yesu alitembea kwenye njia za vumbi, alijivuta matopeni akivuka mito, aligusa mikono michafu ya watu maelfu.  Alipindua meza na hata kupindua mapokeo ya kale … na hata kifo akakipindua. 

Je!, Maisha kama haya, yanasikika kweli kuwa maisha ya utulivu na ya utaratibu?  Wala! Mtu akiamua kumfuata Yesu ajue hiki: maisha yatachafuka kwa matata ya kutosha. 

Inabidi uyazoee.  Ndio gharama ya kutenda kazi ya Ufalme. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly