Matazamio Makubwa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 6:14,15 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
Matukio yaliyotokea zamani, miaka elfu mbili iliyopita, na matukio ambayo tunaenda kusherehekea baada ya siku chake yanayohusu “Krismasi”, je! Yana uhusiano gani na maisha yetu katika karne hii ya 21?
Siku hizi chache zilizopita, tuliona namna ambavyo wana wa Israeli walielewa vibaya ujio wa Masihi wao ulimwenguni, Yesu, Mwana wa Mungu kwa kuwa walikuwa wameufafanua tofauti kabisa.
Walitazamia kupata mfalme shujaa mpiganaji ambaye angewafukuza Warumi watoke kabisa katika Nchi ya Ahadi; walitazamia Masihi ambaye angewaokoa na mazingira magumu. Lakini Mungu alikuwa ameandaa kutenda makuu zaidi. Aliwatumia Mwanae, awaokoa na dhambi zao.
Lakini baada ya Yesu kuhubiri kwa uwezo na kuponya watu kimuujiza, bado hawakuelewa!
Yohana 6:14,15 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
Unaona? Bado walitaka kumlazimisha awe mfalme ambaye angeenda sambamba na matazamio yao, awaokoe kutoka kwenye mazingira yao. Sasa Yesu alikuwa na mwitikio gani? Alijitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake
Ni mara ngapi na sisi tunafanya kitu kama hicho? Mungu, niokoe na tatizo hili. Mungu, tumia mazingaombwe yako uniokoe na hilo.
Ni kweli, Mungu anajishughulisha na maisha yetu, kwa kuwa anatupenda. Lakini shabaha ya Yesu kuja ilikuwa ni kutuokoa na dhambi zetu. Ili ukimwamini tu, usipotee, bali upokee karama bure ya uzima wa milele. Ninakusihi, acha akutendee kama alivyokusudia.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.