... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mbinu ya Kuamini

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 3:16,17 Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Listen to the radio broadcast of

Mbinu ya Kuamini


Download audio file

Sisi sote kwa kiwango fulani, ni kama tunavaa miwani yenye rangi, ina maana, tunaona mambo kwa mtazamo wetu, ukitiwa rangi na matukio tuliyoyapitia.

Tabia ya kuchuja mambo ili kujua ni yapi yanatupendeza kwa dhana ya kutafuta ukweli, ni hatari. na ndio maana kwenye kesi kubwa, waendesha mashtaka na mawakili wa utetezi wa pande zote mbili huwa wako makini sana kwenye uteuzi wa baraza la mahakama.  Hawataki watu wakate kesi mitazamo yao. 

Lakini kuna kitu hakijadhihirishwa kama inavyotakiwa, Ni tabia ya sisi tunaojiita “Wakristo” kuchuja yale tunayosoma kwenye Biblia.  Kama vile Stephen Covey alivyoandika kwenye kitabu chake maarufu kuhusu biashara kiitwacho“Tabia Saba Ya Watu Wanaoleta Matokeo Yanayotarajiwa”: Watu wanasema mtu huwa anaamini yale aliyoyaona. Lakini ukweli ni kwamba imani ndiyo inayochuja yale aliyoyaona.  Yale tuliyokuwa tunayaamini, 

Hivyo ndivyo tunavyosoma Biblia.  Kuna msemo wa mtu fulani, sikumbuki niliupata wapi, lakini alisema hivi:  Wakati unasoma Neno la Mungu, usisome tu yale unayoyaamini.  Wewe Amini yale unayoyasoma.  

2 Timotheo 3:16,17  Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 

Ulifuata vizuri?  Kila andiko ni pumzi ya Mungu.  Kwahiyo unaposoma Biblia, usisome tu yale unayoyaamini.  Wewe Amini yale unayosoma. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy