Mlinzi Wako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 18:1,2 Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Usalama wa mtu ni hitaji la msingi, Linafuata mahitaji mengine muhimu kama vile kuvuta pumzi na kadhalika. Kuna wakati usalama ni wa muhimu kuliko mahitaji mengine ya msingi kama vile maji, chakula, hifadhi na nguo.
Mimi kama mtu aliyefunzwa mbinu za kivita, naweza kukwambia kwamba wanajeshi wakichimba handaki kwa kuandaa eneo la kujihami, ni kwa kuhakikisha usalama wao. Tulinung’unika wakati wa mazoezi baada ya kutembea umbel mrefu kufanya maigizo ya vita, ilitubidi tuchimbe handaki zile kabla ya kupewa nafasi ya kupumzika na kulala. Lakini walipotuonyesha namna ambavyo mizinga mikubwa na ndege za kivita zinavyoweza kuteketeza milima yenye mahandaki, hatukulalamika tena!
Kuna wakati tunahitaji ulinzi, – ulinzi wa kimwili, wa kihisia na wa kiroho pia. Kijana Daudi kabla hajasimikwa kuwa mfalme wa Israeli aliwindwa na mfalme Sauli aliyetaka kumuua. Baada ya kuokolewa na maadui, Daudi alitunga maneno yafuatayo:
Zaburi 18:1,2 Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Maneno yake yalitokana na mambo mengi machungu aliyoyapitia Daudi. Katikati ya mapambano yale, aligundua uaminifu wa Mungu. Kwa hiyo makombora ya mizinga mikubwa ikianza kukuangukia katika, ndege za kivita zikianza kuachia mabomu, hata iweje, nataka ujue yafuatayo:
BWANA ni jabali yako, na boma lako, na mwokozi wako, Mungu wako, mwamba wako unayemkimbilia, ngao yako, na pembe ya wokovu wako, na ngome yako. Usisahau hayo, kwa sababu …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.