... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mpango Usioeleweka

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 1:29-35 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hlli, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Mpango Usioeleweka

Download audio file

Kwa kweli, sherehe hii iitwayo Krismasi inachanganya mawazo ya watu.  Wengine wanaisherehekea kwa kupamba miti ya saipres na kula nyama ya batamzinga. Yaani mapokeo ni mengi tu tena tofauti-tofauti. Labda watu wanafanya hivyo kwasababu hawaelewi maana halisi ya Krismasi.

Mimi binafsi ninafikiri kwamba Krismasi imekuwa desturi tu kwa watu wengi, yaani inakuwa sababu ya kufanya sherehe bila kuelewa maana yake. Lakini hali hii isingetushangaza. Kwasababu zamani hata Mariamu hakuelewa kilichokuwa kinaendelea:

Luka 1:29-35  Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?  Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.  Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.  Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.  Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.  Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hlli, maana sijui mume?  Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. 

Ilikuwa vigumu sana kuelewa lakini mawazo ya Mungu hayako kama mawazo yetu.  Njia zetu si kama njia zake.  Anafanya mambo kwa njia isiyotazamiwa, lakini hiyo si sababu ya kukwepa maana halisi ya Krismasi na kusherehekea sikukuu bila hata kufikiria habari za Kristo. 

Habari Njema ni kwamba, Yesu alikuja kwa ajili yako.  Alikuja kwa njia isiyotazamiwa ili atende kazi isiyotazamiwa.  Alikuja kukuokoa na dhambi zako.  Alikuja ili akupe karama ya uzima wa milele.  mwamini Yeye. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy