... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mpendane Ninyi kwa Ninyi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 13:34,35 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Mpendane Ninyi kwa Ninyi


Download audio file

Kupenda watu unaopendezwa nao ni rahisi sana – hata kama mahusiano yenu yanaweza kuwa na visiki na vikwazo mara kwa mara.  Lakini kwa upande mwingine, kupenda watu usiopendezwa nao si rahisi, hmm!, niwapende kweli? Kwani ni lazima niwapende?  Nafikiri umeshanielewa.

Si chini ya mara kumi na tatu Agano Jipya limetuambia tupendane tena kwa upendo thabiti usio na masharti.  Ni Yesu mwenyewe alituagiza hivyo: 

Yohana 13:34,35  Amri mpya nawapa, Mpendane.  Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.  Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. 

Ni kweli, hata Agano la Kale linaongea habari za namna inavyotupasa kutendea watu wengine, lakini Yesu ndiye aliyelikaza zaidi swala hilo kiasi ambacho analiita “amri mpya”. Hadi akasema kwamba kumpenda Mungu na moyo wako wote na kumpenda jirani kama unavyojipenda hiyo inajumuisha Torati nzima ya Wayahudi na hata maneno ya Manabii. 

kweli, kule kupendana kama Yesu alivyotupenda siku alipokufa kwa ajili ya dhambi zetu, yeye anasema hiyo ni dalili ya kwamba mtu ni Mkristo wa kweli.  

Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.  

Hapa hatuna somo la kinadharia, hii inahusu namna mimi na wewe tunavyowapenda wanaotuzunguka.  Tunaweza kuwa wavivu kupenda hata wale wanaotupendeza, sembuse kufanya ile kazi ngumu ya kuwapenda wasiotupendeza na kutuchukiza!?. 

Amri mpya nawapa, Mpendane.  Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy