... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ukarimu na Ushirikiano

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Matendo 2:46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe.

Listen to the radio broadcast of

Ukarimu na Ushirikiano


Download audio file

Nataka nikuulize, wewe ukisikia neno “kanisa” unawaza nini?  Ni jengo? (wengi wanafikiri hivyo). Au kanisa ni utaratibu wa ibada unayoihudhuria kila jumapili?  Ni taasisi, familia au? … niambie, “kanisa” lina maana gani kwako?

Siku hizi, mtazamo wa mapokeo ya zamani kuhusu kanisa, ni kama yameachwa na wengi. Watu wa Mungu wengine wanapelekwa huku na huko.  Wengine wanasema kwamba hawataki kuendelea kuigiza tu. Wengine watakwambia kwamba waliumizwa vibaya kanisani. Janga la korona imechangia kusambaza waumini, ahahahaa. 

Wewe vipi?  “Kanisa” lina maana gani kwako?  Una mahusiano gani na familia ya wanaomwamini Yesu Kristo?  Wakati bado unatafakari maswali hayo kichwani, ebu tuangalie ilivyokuwa katika kanisa la kwanza: 

Matendo 2:46  Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe. 

Mara kumi na tatu tunaambiwa ndani ya Agano Jipya kwamba waamini walikusanyika “nyumba kwa nyumba”, au kwa Kornelio, au kwa Mariamu au kwa Lidiya, au nyumbani mwa mlinzi wa gereza na kadhalika. 

Hata mkusanyikaje kuna mambo matatu hampaswi kuyasahau kama wafuasi wa Yesu Kristo. 

Kwanza, muwe na lengo maalum mnalounganika kwalo, ukiwa na ndugu; yaani lengo la kutiana moyo katika imani; lengo la kuwaambia wengine habari za Yesu.  Pili, kuchukua nafasi ya kutosha kukaa pamoja, na tatu, ni muhimu, kuchangia chakula, mkialikana kula pamoja kwa furaha na moyo mweupe. 

Ni kweli, kukusanyika kama kanisa ni kwa ajili ya kuabudu, ni kwa ajili ya kufundishwa, lakini pia, kanisa ni kuondoa unafiki, kukutana kama familia na kuwa na malengo la pamoja. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.