... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mwachie Bwana Nafasi ya Kutenda

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 34:6-9 Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, akamwokoa na taabu zake zote. Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa. Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; heri mtu yule anayemtumaini. Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, yaani, wamchao hawahitaji kitu.

Listen to the radio broadcast of

Mwachie Bwana Nafasi ya Kutenda


Download audio file

Ebu fikiria kana kwamba unachimba alimasi.  Mwezi baada ya mwingine unajichosha kabisa na kukatishwa tamaa na kazi ngumu mno bila mafanikio.  Hamna kitu.  Kwa hiyo, siku moja unaamua kuacha na kuondoka.  Lakini bila wewe kujua, kumbe!  Ulikuwa umekaribia kwa inchi cache kufikia kitovu cha alimasi. 

Hadithi yako ni nzuri, utasema moyoni mwako, lakini mimi sijioni kuwa mtu anayeweza kuchimba alimasi au dhahabu au vito vya thamani.  Hiyo siyo kipaji changu wala wito wangu.  Sawa, uko sahihi. 

Lakini ni mara ngapi twaweza kujikuta sehemu gumu, labda kazini kukimtumikia bosi mkali, au uhusiano fulani unaoyumba, au hali duni la uchumi, au hali ingine awaye yote … halafu tunamwomba Mungu, na kumwomba na kuendelea kumwomba bila jibu au mafanikio yo yote? 

Kwa hiyo, siku fulani tunaacha na kuondoka.  Lakini sikiliza tena alivyotamka Daudi, mfalme wa Israeli katika uzoefu wake: 

Zaburi 34:6-9  Maskini huyu aliita, BWANA  akasikia, akamwokoa na taabu zake zote.  Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.  Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; heri mtu yule anayemtumaini.  Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, yaani, wamchao hawahitaji kitu. 

Mara nyingi, Mungu hua anatenda kazi kisiri-siri, hata kabla hatujamwomba.  Malaika zake wanapiga kambi kwa kutuzungukia na kutulinda.  Ni kweli kabisa!  Sasa Daudi anatutia moyo, wewe na mimi, muda ule tunapochoshwa mno na kutaka kuacha na kuondoka.  

Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; heri mtu yule anayemtumaini. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy