Mwaka Umeisha Sasa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 43:18,19 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
Haya! Tumefika sasa kwenye tarehe 31 ya Desemba, siku ya kuamkia Sikukuu ya Mwaka Mpya. Leo ni siku ya mwisho wa mwaka huu. Ifikapo saa sita ya usiku, basi utakuwa umeisha.
Hata hivi, kwa mwisho kabisa wa mwaka huu, kuna wengi wataruhusu maumivu na makosa ya mwaka huu kuendelea kuwadhuru hata ndani ya mwaka mpya mpaka ndani ya miaka inayofuata. Kinachohuzunisha zaidi ni kwamba kati ya watu hawa, kuna baadhi yao ni watu wa Mungu, wenye kumwamini Yesu na mioyo yao yote.
Labda kuna kitu kilichotokea mwaka huu uliopita au hata zamani kama vile majuto, kutokujisamehe, uonevu au hasara fulani ambavyo bado vinakusumbua sana moyoni na kukuathiri kama vile kansa. Kama ni kweli, basi unahitaji uwezo wa ki-Mungu kukuweka huru. Uwezo wa Roho Mtakatifu kuvunja minyororo inayokufunga. Sikiliza hii
Isaya 43:18,19 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
Mungu alitamka Neno lake kwa wana wa Israeli kipindi kigumu sana wakati walikuwa wamepelekwa uhamishoni kama watumwa. Alikuwa amewaadhibu hivyo kwa sababu ya uasi wao, na jinsi walitenda dhambi na kuabudu sanamu.
Nisikilize – bora umsikilize Mungu. Kwa nguvu ya Roho yake, sahau yaliyopita. Usitafakari mambo ya zamani. Yeye ameanza kutenda mambo mapya … ndani yako na kupitia wewe. Bila shaka unajua kwamba hii ni kweli, kwa sababu …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.