U Wapi, Ewe Mauti, Kushinda Kwako?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 15:54-58 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Dunia hii imejaa maumivu mioyoni mwetu na hata ndani ya mwili huu unaozeheka na kuelekea hatima yake. Kwa ufupi kuna mambo yanaumiza kihisia.
Bila shaka umewahi kupitia kipindi kigumu maishani mwako, wakati ukiona kila kitu kinaharibika, kipindi hicho kigumu hatimaye kinapita na mtu anajikwamua. Lakini kadiri mtu anazeeka, mwisho wake ni kifo.
Lakini kama unamwamini Yesu siyo hivyo.
1 Wakorintho 15:54-58 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Kwahiyo siku utakayojisikia ya kwamba unatereza na kuporomoka jua hili: Tangu ulipoweka Imani yako kwa Yesu, na kupata ushindi wa milele jua umauti umekungojea. Kwa hiyo rafiki yangu, simama imara. Yote unayoyafanya, uyafanye kwa ajili ya Bwana. Haitakuwa kazi bure.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.