... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ninavyofikiri Mimi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.

Listen to the radio broadcast of

Ninavyofikiri Mimi


Download audio file

Kila mtu ana maoni yake kuhusu mambo mengi tu. Kuhusu yaliyo mema na mabaya, kuhusu siasa, kuhusu watu mashuhuri. Tuna maoni ya kukosoa wake zetu, waume zetu, majirani zetu.  Yaani sisi sote tuna maoni mengi tu!

Kadiri ninavyoangalia vyombo vya habari, hususani kwenye mtandao ndivyo ninavyozidi kutambua kwamba habari hizo si taarifa za matukio hasa, bali ni habari za maoni ya watu tu. 

Sasa, ni kawaida mtu kuwa na maoni yake na si kila oni ni baya, hapana.  Lakini ebu fikiria kwanza matokeo pale tunapokuwa na msimamo juu ya mtu fulani au kitu fulani, pale tunapojenga maoni. Ni kama tunajifanya kuwa mahakimu na baraza la wazee au watekelezaji wa hukumu.

Hata watu wa Mungu wengi – wale waliochanganyikiwa kwa kujiita Wakristo – wana maoni yao juu ya Neno la Mungu.  “Wala sikipendi kipengele hicho, kiache tu.”  Kwa hiyo kila mmoja anakaa kivyakevyake akijitenga na wengine katika sera zake na maoni yake ambayo mara nyingi hayako sahihi.  Muda umewadia wa kuamka sasa: 

2 Timotheo 3:16  Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki. 

Je!, Ni nani aliyetupa Maandiko?  Si Mungu mwenyewe? Je!, Ni sehemu gani ya Maandiko inayotufaa kwenye maisha yetu?  Ni sehemu zote!?, sikiliza  Maandiko sio maoni ya Mungu, bali ni ukweli kabisa wa Mungu. 

Kwahiyo niulize, je! Utafuata kweli yake hata kama kuna wakati inasumbua, au utafuata maoni yako tu? 

Ni rahisi kuwa na maoni, bali kukata shauri na kufanya maamuzi sio rahisi. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.