Njoo Unywe
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 7:37,38 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
Je!, Umewahi kuamka asubuhi na kujikuta kwamba imani yako ndani ya Kristo ni kama imekauka na kuna ukame ndani yako ukitambua kwamba imani imepungua sana? Bila shaka umewahi kujisikia hivyo – hata mimi! Lakini, swali lilopo ni hili, mtu atafanya nini?
Sijui wewe inakuaje, lakini kwangu mimi, kuna wakati maisha yanakuwa bize sana, mtu anachoka mno, na mahusiano yale na Yesu yalikuwa mazuri na yenye kusisimka, lakini yakiwa makavu hayatakiwi kuwa hivyo.
Hukukusudia iwe hivyo. Hukupanga ibadilike hivyo. Lakini maisha haya huwa yana tabia ya kukunyonya hadi mahusiano yako na Bwana wako yanakaushwa kabisa – kwa vyovyote inasikika hivyo.
Matokeo ni kwamba, furaha uliyokuwa nayo inatoweka. Yale uliyoweza kufanya kwa jina lake hapo awali, ukitumia vipawa ulivyopewa na Mungu ukihudumia watu wanaokuzunguka, sasa yanakuwia vigumu sana kuyatimiza. Lazima kitu kimoja au kingine kilegee. Ndipo Yesu anakuonekania:
Yohana 7:37,38 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
Jibu linaloweza kupatikana sehemu ile ya ukame, yaani dawa ya kiu uliyo nayo, ni Yesu mwenyewe. Je! Una kiu? unywe maji ya uzima, bali hadi pale umejaa tele Roho yake kiasi cha kufurika tele kama mto unaotoka ndani yako.
Kama vile mtu fulani aliwahi kusema, ukimwendea Yesu kupata maji ya kunywa, maji yale yanabadilika kuwa kama mto, au kama mito kabisa. Uje kwa Yesu, unywe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.