... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Nyuki Mchapa Kazi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 15:8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.

Listen to the radio broadcast of

Nyuki Mchapa Kazi


Download audio file

Zamani nilifikiri kwamba lengo la maisha ni kujifurahisha tu, Sikiliza, wazo hilo lilinipelekea kutaka kujinyonga.  Kumbe kuna lengo lingine ambalo lina thamani kubwa kuliko kujifurahisha.

Kwa kawaida, nyuki anaishi siku arobaini tu.  Na katika maisha yake hayo mafupi anatembelea maua zaidi ya elfu moja akitengeneza asali inayopungua kidogo kutimia kijiko kimoja. Sisi tunaona ni asali kidogo lakini kwa nyuki ni kazi ya maisha yake yote.  Kijiko kile cha asali ni thibitisho la maisha yanayozaa matunda. 

Yule nyuki aliumbwa ili akusanye chavua ile kweney maua na kutengeneza asali.  Na sisi pia, wewe na mimi, tumeumbwa na Muumba aliye makini sana ili tuweze kutimiza yale aliyekusudia tuyafanye. 

Kwa hiyo tunaweza kuendana na mpango wake na kuishi maisha inayozaa matunda, au tunaweza kutapanya maisha yetu kwa kutafuta kujifurahisha tu.  Yesu alisema hivi: 

Yohana 15:8  Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 

Kwa maneno mengine, lengo lake kwa ajili ya maisha yako na yangu pia ni kwamba tuishi kwa kuzaa matunda.  Ni kweli, matendo utakayozaa yatatofautiana na matunda yangu kwa sababu ametuumba kila mmoja kwa malengo tofauti-tofauti.  Lakini, kwa vyo vyote, hata lengo la kila mmoja likiweje, ukweli ni kwamba matunda tunayozaa ni kwa ajili ya manufaa ya watu wengine. 

Asali ya nyuki ni kwa ajili ya mzinga.  Matunda yako ni kwa ajili yangu.  Matunda yangu ni kwa ajili yako.  Kinachonipendeza mno ni kujua kwamba mtu ataridhika kabisa akizaa matunda yale aliyokusudiwa azae wakati Mungu alimuumba.  Na kule kuridhika kuna thamani kubwa kulika kufurahishwa tu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy