Sahau Yote, Isipokuwa …
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 2:1,2 Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.
Bila shaka, una mambo mengi yanayoendelea maishani mwako muda huu. Yanayopendeza na yanayohuzunisha pia, yaliyo mema na mabaya, yanayostarehesha na mengine yanayochanganya … hayo yote yameteka fikra zako hadi siku utakapolala, yaani kufa.
Nina rafiki wanaojiuliza juu ya yale ninayoyafanya, hawasemi mengi, lakini ninaweza kuhisi wanavyofikiri, “Kwanini umeacha kazi yako ya ufundi mitambo iliyokuwa inakuingizia pesa nyingi na kuanza kujaribu kuwafanya watu wakubali dini yako?”
Kwanza, ningetaka watu wajue kwamba mimi si mtu wa “dini” na silazimishi watu kukubali ninayoyasema.
Kwa mafupi ni hivi: kuna watu wengi sana duniani wanapambana na maisha, wamekosa tumaini, wanaenda kasi wakielekea kutengwa na Mungu milele, huku upendo wake wa ajabu kwa ajili ya kila mmoja wao uko tayari kuwakumbatia.
Ninajisikia kuwa kama Mtume Paulo pale alipowaandikia rafiki zake kwa kanisa la Korintho zamani kwenye karne ya kwanza:
1 Wakorintho 2:1,2 Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.
Katikati ya pirika zote zilizomo maishani mwako, tulia kwanza na kuziweka kando … isipokuwa kukumbuka ukubwa wa ajabu wa upendo wa Mungu kwako kupitia Yesu Kristo na kifo chake pale msalabani.
HIcho ndio kiwango Mungu anachokupendea.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.