... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Umefikia Wapi?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:30,31 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima ya Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

Listen to the radio broadcast of

Umefikia Wapi?


Download audio file

Siju ikama untaniruhusu nikuulize moja kwa moja lakini kwa upole, Umefikia wapi katika swala la imani yako ndani ya Yesu?  Je!, uko kinyume chake kabisa, au uko vuguvugu tu, au unamchangamkia? Naomba unikubalie nikushirikishe habari fulani leo.

Zamani nilikuwa kinyume kabisa, niliwachukia Wakristo kabisa kabisa.  Nilijihesabia haki kana kwamba nilijua kila kitu. nilikuwa na pesa, nilikuwa nilijulikana, nilikuwa na mafanikio. Hivyo, Sikuwa na haja ya gongo la kutegemea, yaani msaada hadi pale maisha yangu yaliponiharibikia, hadi pale niliposimama kwenye ghorofa ya nane nikiwa tayari kujitupa chini ili nife.  

Yesu alinionekania mahali pale pa hatari nikiwa peke yangu, Sasa kitu ninachotaka kukwambia leo ni hiki, upendo wa Mungu kwako ni mkubwa mno. 

Kwasababu, kama alivyonifanyia mimi, anataka sana kukuokoa na mapungufu yako na makosa yako na “dhambi” zako.  Ndio maana alimtuma Mwanae wa pekee, afe msalabani ili alipe deni la “dhambi” zako, deni lililodaiwa na haki yake. Sasa ukiamini kwamba anaweza kukuokoa, sikiliza yanayofuata … 

1 Wakorintho 1:30,31  Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima ya Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana. 

Mwisho wa siku inakuaje?  Yesu anabadilisha kila kitu.  Anamchukua mtu mwenye kiburi kama mimi niliyekuwa nimesimama kwenye lindi kuu la lakukatishwa tamaa kabisa na kunileta leo hapa nilipo ili niweze kukusihi na wewe. 

Weka imani yako ndani ya Yesu … kwasababu yeye anabadilisha kila kitu! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.