... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wateule

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:26-29 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Wateule

Download audio file

Laiti siku moja tungeinua macho yetu na kutafakari ulimwengu mzima na kujitambua kwamba sisi ni wadogo sana; jinsi sayiri yetu, yaani dunia hii inavyolizunguka jua kwa kasi, jua ambalo ni nyota ndogo sana kuliko nyota zote.

Taswira hiyo inaweza kutusaidia! Sasa katika binadamu wote wanaoishi duniani, kuna wengi wanatuzidi sisi, akili, cheo, mali.  Je! inawezekana kweli Mungu mwenye uweza wote, mwenye upendo wote … atujali sisi, watu kama wewe na mimi? 

Kwa kweli, nina habari njema kwako, kama unamwamini Yesu kweli kweli, kama unaambatana na Msalaba wa Kristo kupitia mapungufu na mawimbi ya maisha haya, basi wewe ni mwanae mteule. 

1 Wakorintho 1:26-29  Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 

Kwa mtazamo wa ulimwengu huu, Yesu alionekana kuwa mpumbavu pale alipotundikwa Msalabani. Hata sisi pia tunaonekana kuwa wapumbavu machoni pa ulimwengu pale tunamwamini Yesu. Lakini tukimwamini, tumeteuliwa kuwa watu wake katika ulimwengu mzima. Tafakari kweli hiyo!  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.