... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Upumbavu na Udhaifu wa Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakorintho 1:22-25 Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima, bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

Listen to the radio broadcast of

Upumbavu na Udhaifu wa Mungu

Download audio file

Mimi binafsi ningependelea Mungu afuatane na matazamio yangU; na kutenda kama ninavyotaka,Wewe, vipi?  Lakini kusema ukweli Mungu hafanyi hivyo hata kidogo.  Kumbe, ukiangalia matokeo, ni bora asitubembeleze.

Kwa hiyo tuulize … kwa nini Mungu amejificha machoni petu?  Kwanini asijidhihirishe kwa kila mtu waziwazi, atupange vizuri, atufanye tukae pamoja?

Wazo hilo linaeleweka, Nadhani wewe na mimi tungefanya hivyo, Kama tungekuwa na uwezo wote wa Mungu pamoja na upendo wake, tungeingilia kati na kukomesha machafuko yaliyomo duniani mara moja tu, basi. 

Wakorintho 1:22-25  Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima, bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.  Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu. 

Kumbe!, Tayari Mungu amefanya, hata kama inaonekana kuwa upumbavu kwa watu baadhi. Amejidhihirishia kila mtu duniani, ameandaa njia ya kutatua matatizo yote. Ameachilia uweza wake ili tukae pamoja kwa amani … lakini kwa njia ya upendo inayompa kila mmoja wetu kukata shauri. 

NI uamuzi wako kumwamini Yesu, lakini  Yeye ndiye njia; njia pekee. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.