Matazamio Yenye Shauku
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 15:23,24 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
Mambo yanayoendelea katika maisha yetu, wewe na mimi yana nguvu sana, Yanajenga mazingira yetu kabisa na kufupisha mtazamo wetu kuhusu umilele na kusababisha tuangalie yaliyopo mbele yetu tu kwa muda huu huu!
Ni kweli, kama humwamini Yesu, ninaelewa vizuri ni kwanini huna muda wa kutafakari habari za umilele. Lakini kama unamwamini Yesu kama mimi ninavyomwamini, naona kwamba ni tatizo endapo utakuwa huna muda wakufikiria sana kuhusu maisha ya milele. Kwasababu maisha yetu tutakayoishi milele ndani ya Yesu ni maisha ya ajabu mno.
1 Wakorintho 15:23,24 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
Siku moja mwisho wa dunia utafika, au tutakufa; wewe na mimi, au yawezekana pia Yesu akarudi tukiwa bado tuko hai. Halafu watawala wote, na mamlaka zote pamoja na nguvu zote hata mazingira yote ya kisasa yatatoweka kabisa! Ebu fikiria hayo!
Halafu walio wake Kristo, atakapokuja watafufuliwa.
Kama unamwamini Yesu, hii ndiyo hatima yako. Hii ni hali halisi yako. Usiruhusu mambo yaliyopo sasa hivi yakuibie matazamio yako yenye shauku.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.