Je! Ni Akina Nani Mungu Anayewasikiliza?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Malaki 3:16 Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.
Katika historia ya Israeli wakati wana wa Israeli walipomuasi Mungu na kumpa kisogo walikuwa wanapata matokeo ya uasi wao dhidi yake. Je! umeishapitia hali kama hiyo?
Haujambo? Mimi ni Berni Dymet ninakukaribisha kwenye kipindi hiki cha NENO SAFI NA LENYE AFYA.
Bila shaka umeshaona kwa sababu sisi sote tumepitia kipindi kama hicho. Sote tumewahi kumwacha Mungu na kama vile mtoto aliyeasi hana budi kupata matokeo, na sisi kutokutii kwetu na uasi wetu dhidi ya Mungu lazima tupate matokeo.
Mtu hawezi kuishi katika amani, hawezi kujazwa na furaha ya Bwana wakati amemuasi. Mungu ndiye alipanga iwe hivyo. Matokeo yale, maumivu yanayotokana na uasi wetu … yamekusudiwa kutushtua, kutuamsha ili tuweze kumrudia Bwana.
Tukirejea kwa habari ya Israel, tunaweza kuuliza, je! Waliamkaje? Waliwezaje kupata tena usikivu wake Mungu?
Malaki 3:16 Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.
Je! Ni nani Mungu atawasikiliza? Ni wale ambao waliomcha, wale ambao katika lugha ya asili ya Kiebrania walimwogopa, Ni wale waliomheshimu na ambao waliolitafakari jina lake.
Yamkini umepitia kipindi cha maasi. Labda umemwacha Mungu na sasa uko mbali naye. Nisikilize. Bado unaweza ukumrudia, Daima yu tayari kuwasikiliza wale wanaomwogopa na kumcha, wale ambao wanataka kuliheshimu jina lake. Hujapitwa na wakati.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.
Je! Umewahi kuwa na hisia ya kutamani watu wakuheshimu zaidi? Matamanio ujulikana zaidi na kupongezwa, kwa tabia yako na kwa yale uliyoyafanya? Ukitamani hivyo, jua kwamba umeanza kupitia njia ya hatari,
Hujambo? Mimi ni Berni Dymet ninakukaribisha kwenye kipindi hiki cha NENO SAFI NA LENYE AFYA.
Mimi sidhani kwamba kuna mtu anaweza kuwa na kiburi kidogo tu. Kiburi hua kinakua na kuvimba haraka sana. Bila hata kufikiria, shauku ile ya kutambulika zaidi itammeza mtu yule anayetamani kuheshimika: ataanza kufikiri ni haki yake kutukuzwa.
Wala. Hakuna mtu awezaye kuwa na kiburi kidogo tu.
Kanisa la Korintho kwenye karne ya kwanza liligawanyika na ugomvi uliotokana na kiburi cha watu waliodai haki ya kutambulika. Kwa hiyo Mtume Paulo aliwaandikia barua kali.
1 Wakorintho 5:6,7 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.
Ni mfano mzuri sana. Chachu kidogo kinachachusha donge zima na kusababisha ivimbe kabisa. Kwa hiyo inabidi tutupe donge zima na kuanza upya bila chachu. Hata kidogo.
Kiburi kile kidogo hakina nafasi katika maisha ya mtu ambaye anataka kumfuata Yesu. Kitupe nje. Anza upya.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.