... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kiburi Kidogo Tu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 5:6,7 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amrkwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Kiburi Kidogo Tu


Download audio file

Je!  Umewahi kuwa na hisia ya kutamani watu wakuheshimu zaidi?  Matamanio ujulikana zaidi na kupongezwa, kwa tabia yako na kwa yale uliyoyafanya?  Ukitamani hivyo, jua kwamba umeanza kupitia njia ya hatari, 

Mimi sidhani kwamba kuna mtu anaweza kuwa na kiburi kidogo tu.  Kiburi hua kinakua na kuvimba haraka sana.  Bila hata kufikiria, shauku ile ya kutambulika zaidi itammeza mtu yule anayetamani kuheshimika: ataanza kufikiri ni haki yake kutukuzwa. 

Wala.  Hakuna mtu awezaye kuwa na kiburi kidogo tu. 

Kanisa la Korintho kwenye karne ya kwanza liligawanyika na ugomvi uliotokana na kiburi cha watu waliodai haki ya kutambulika.  Kwa hiyo Mtume Paulo aliwaandikia barua kali.  

1 Wakorintho 5:6,7  Kujisifu kwenu si kuzuri.  Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?  Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu.  Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo. 

Ni mfano mzuri sana.  Chachu kidogo kinachachusha donge zima na kusababisha ivimbe kabisa. Kwa hiyo inabidi tutupe donge zima na kuanza upya bila chachu.  Hata kidogo. 

Kiburi kile kidogo hakina nafasi katika maisha ya mtu ambaye anataka kumfuata Yesu. Kitupe nje.  Anza upya.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.