Tunakuombea
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wathesalonike 3:5 Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.
Leo nataka kukamilisha masimulizi kuhusi namna tunavyoanda kipindi hiki cha kuchochea moyo wa ibada ndani yako kila siku. Nina jambo ambalo si la kawaida la kukwambia linalotoka ndani ya Neno la Mungu, kwa sababu Mungu anampango wakupindua na kubadilisha maisha yako.
Kila asubuhi ninapokaa mbele ya komputa yangu ili niandike ujumbe kutoka kwenye Neno la Mungu, nakwambia kwamba, huwa kuna mafuriko ya furaha moyoni mwangu kwa fursa nzuri niliyonayo yakukushirikisha mambo ya Kristo.
Mara nyingi kwasababu ya udhaifu katika mwili na kupambana na upepo mkali wa maisha, inakuwa si rahisi kuendelea kufurahia kazi hiyo; lakini Roho Mtakatifu ananionekania na kunijaza bidii ya kuendelea na safari hii tukiwa pamoja kwa kuchunguza Neno lake. Na Neno lake ndilo linaloweza kubadilisha maisha yako kwa utukufu wa Kristo. Kwa hiyo hapa kwenye huduma yetu ya Christianityworks (Ukristo unafanyakazi) …
2 Wathesalonike 3:5 Tunawaombea ili Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.
Mungu anataka wewe mwenyewe uelewe na kujua fadhili alizo nazo kwa ajili yako. Anataka uishi maisha kwa saburi ile ile aliyokuwa nayo Yesu alipoishi hapa duniani na kustahimili mpaka pale alipoweza kufa kwa ajili yako. Kufanya hivyo, inatakiwa uwe na uwezo. Inatakiwa uwe na uwepo wa Roho ndani yako. Inatakiwa kweli ya Biblia iandikwe moyoni mwako.
Tunawaombea ili Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.
Niruhusu tafadhali nikutie moyo kufungua moyo wako kupokea Neno la Mungu, hata kama kuna siku maagizo yake yanakuwia magumu. Wewe Yasikilize, yeye anataka abadilishe maisha yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.