Ubia Wenye Nguvu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 4:21-24 Ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Ni nani asiye na nia ya kuishi maisha bora? Maisha iliyowekwa huru na makosa aliyoyafanya zamani, maisha yanayoweza kutikisa ulimwengu kwa kuleta mema. Yaani ni shauku ya asili inayokuwa moyoni mwa mtu.
Lakini shida iliyopo ni kwamba ili mtu ashike uzima ule bora, lazima abadilike, awajibike, ajitolee. Ndio maana wengi sana wanapata hasara, wasiweze kufurahia maisha bora kwa sababu wanaogopa gharama.
Lakini thawabu yenyewe … yaani tuzo kwa yule anayeachana na utu wa kale na kuushika utu mpya, kusema ukweli ni vigumu kueleza namna lilivyo bora. Yaani ni jambo bora mno. Ni hatua inayopendeza kabisa. Ni jambo jema kuliko yote tuliyowahi kuyaishi zamani tulipokuwa tunagaa-gaa kwenye tope la mapungufu yetu na udhuru tulizotoa.
Kusudi la moyo wa Mungu siku ya leo, bila shaka, ni kutusaidia tuinue macho yetu ili tuweze kuona yatakayowezekana tukiingia katika ubia wenye nguvu pamoja naye.
Waefeso 4:21-24 Ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Kwahiyo, niulize, je! Umechagua nini? Kuendelea kuharibika … au kuzidi kuboreka? Katika uzembe wetu, ni rahisi kudanganywa na uovu tunaotaka kufanya. Lakini Mungu Roho Mtakatifu, sasa hivi, yuko tayari kubadilisha mioyo yetu na nia zetu. Kwahiyo … Uwe mtu aliyeumbwa kwa kusudi la kufanana na Mungu, mtu mwema anayempendeza.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.