Jukumu Linalotisha
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Ezekieli 3:18,19 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.
Ni kama kanuni kwenye ulimwengu huu kwamba kila baraka inakuja na jukumu lake. Kwahiyo, kama wewe ni tajiri, ni jukumu lako kuwasadia maskini.
Ikiwa wewe unamwamini Yesu kama vile mimi ninavyomwamini, basi baraka kubwa katika maisha yako ni kuwa na uhakika kwamba kupitia sadaka yake pale Msalabani gharama ya ukombozi uliotafutwa pamoja na haki ya Mungu, tayari vilishalipwa vyote.
Na ukweli huo … umekufungulia mlango kuingia katika maisha mapya, ukiwa huru na madhara ya dhambi, ukiwa na maisha yatakayoendelea mbele za Mungu milele na milele. Je! Kuna baraka kubwa kuliko hiyo,
Lakini pamoja na baraka ile kuna kuja jukumu zito sana. Lisikilize kwa mtazamo wa Mungu mwenyewe:
Ezekieli 3:18,19 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.
Ni jukumu lipi zito? Ni kuwaambia watu unaowajua habari za Yesu. Kuwaambia Habari Njema za baraka kubwa kuliko zote. Je! Wote watakusikiliza? Wala. Je! Wengine watakutenga au kukutukana na kukuudhi kwa sababu umewaonya? Ni kweli kabisa. Lakini wakikukataa, basi damu yao haitakuwa juu yako.
Usidanganyike, kwa kweli ni jukumu zito sana, kila mmoja wetu anayejiita Mkristo anawajibika kwalo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.