... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Udanganyifu wa Kujiona uko Salama tu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yeremia 5:30,31 Jambo la ajabu, la kuchukiza, limetokea katika nchi hii! Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?

Listen to the radio broadcast of

Udanganyifu wa Kujiona uko Salama tu


Download audio file

SIku hizi “ukweli wa ki-Biblia” unachukuliwa kama umeshapitwa na wakati.  Yaani mambo ambayo Wakristo baadhi wanayaamini hayaendani na kasi ya kisasa, kwahiyo wengi wanakubali kupelekwa na mkondo huo wa ulimwengu wetu.

Matamanio yetu ya kuwa na uhakika wa mambo pamoja na usalama ni kawaida kwasababu yanatokana na asili yetu tuliyorithi kama binadamu ili mtu anusurike na aendelee kuishi.  Hata nzi anaasili.  Lakini kwa sisi wanadamu, inaweza kutuletea matokeo tusiyoyatazamia. 

Daktari bingwa aitwaye Mitch Wallis anayeshughulika na afya ya akili alinukuliwa  hivi karibuni akisema hivi,  “ubongo wa mwanadamu unahakikisha usalama wake kuliko kutafuta ukweli uko wapi.” Na ndio maana mwanadamu anapendelea kusikia habari njema kuliko habari mbaya.  Anapendelea vipindi vya furaha kuliko vipindi vya huzuni tuko pamoja, sindiyo? 

Sasa hatari iko wapi?  Hatari ni kwamba, kuna mambo mengine huwa tunayaona kama yako salama nay a uahakika kumbe sio. Maneno tunayoambiwa na watu hasa yale tunayopenda kusikia, kuna wakati yanakuwa si ya kweli. 

Yeremia 5:30,31  Jambo la ajabu, la kuchukiza, limetokea katika nchi hii!  Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo.  Nanyi mtafanya nini mwisho wake? 

Ulimwengu huu unatushawishi tuishi maisha yanayotuvutia kutuvutia    kwamba ni salama salamini. Hata baadhi ya watu katika makanisa hawako tayari tena kusaidia watu wa Mungu katika kutenganisha mema na mabaya. 

Kule kuambiwa na mtu mambo tunayoyapenda kusikia hiyo haifanyi hayo mambo kuwa ya kweli, sasa mtu akiachana na ukweli huyo itakula kwake na ataona matokeo ya hatari. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy