Uhakika na Bayana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Si unapenda kukutana na watu jasiri ambao wana hakika ya mambo, wakijiamini. Ukikaa nao, mara moja utaanza kujisikia kwamba na wewe si mtu wa mashaka tena. Je! Ni kipi kinachowatenganisha watu kama hao?
Maishani mwangu kuna watu kadhaa waliokuwa hivyo. Licha ya matatizo waliyoyaona – na kuna wengine walipitia mengi tu kwa muda mrefu – ni kama hakuna kitu kinachoweza kuwatikisa. Nikitafakari habari zao, nasikia kwamba nimejengeka nafsini mwangu.
Wakati niliwahoji maswali, wakati nilitafiti kwao nipate majibu, kuna jambo moja ambalo daima limejirudi. Ni imani yao. Mara nyingi wanasimulia swala la safari yao ya imani. Sasa neno lile–imani Je! Utalitafsirije? Utawezaje kulishika wewe mwenyewe?
Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Tumepata maneno mawili: hakika na bayana. Hakika kwamba yale ambayo tunayoyatarajia, bayana ya mambo yasiyoonekana. Yanawezekanaje?
Jibu ni rahisi: ni kwa sababu wakati mtu anaweka tumaini lake kwake Yesu, si matumaini yanayoweza kuyumbishwa, hapana. Si matumaini yasiyo na uhakika.
Siri ya kutulia katika hakika na kuwa na bayana ya mambo ni kutembea karibu na Yesu. Kwa sababu, kadiri mtu anazidi kumjua, ndipo imani ndani yake itakapozidi kukua, halafu ndipo uhakika na ujasiri wake utazidi kuwa mkubwa.
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.