... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ukosoaji Usiofaa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Nehemia 4:1,2 Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?

Listen to the radio broadcast of

Ukosoaji Usiofaa


Download audio file

Kuna aina mbili za ukosoaji zinazolingana nguvu na ni lazima utakutana nazo tu kwenye maisha yako – kuna ukosoaji unaojenga na kuna ukosoaji unaobomoa.  Kuna utofauti mkubwa kati ya aina hizi mbili za ukosoaji.

Leo tuna mada inayohusu ukosoaji unaoharibu na kubomoa. Mnamo mwaka 587 kabla ya Kristo, watu wa Babeli (wakiwa na vyombo alivyotumia Mungu kuhukumu watu wake kwasababu ya ibada zao za sanamu), Wababeli walibomoa mji wa Yerusalemu na kuwapeleka wayahudi utumwani miaka sabini. Sasa Mungu alipowaweka huru na kuwarejesha kwenye Nchi ya Ahadi, kazi yao ya kwanza ilikuwa ni kujenga tena ukuta kuzunguka Yerusalemu. 

Yaani ilikuwa ni mradi mkubwa ulioongozwa na Nehemia.  Lakini walikabiliana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa maadui wao. 

Nehemia 4:1,2  Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.  Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje?  Je!  Watajifanyizia boma?  Watatoa dhabihu?  Au watamaliza katika siku moja?  Je!  Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? 

Bila shaka hata wewe ilipokusudia kutenda mema, ulikabiliana na ukosoaji kama huo. Lakini kinachovutia ni kwamba, ule ukosoaji ulitoka kwa watu waliokuwa wanakaa bure tu, mchezaji wa filamu Denzel Washington aliwahi kusema hivi: 

Kamwe hautakosolewa na mtu anayekuzidi kufanya kazi. Kila utakapokosolewa na mtu asiyefanya kazi kama yako. Yakumbuke maneno hayo. 

Usiruhusu ukosoaji unaobomoa kukustopisha kuendelea kufanya kazi ya Mungu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy