... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ukweli wa Mambo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Malaki 3:13-17 Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani? Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi? Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao. Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake. Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.

Listen to the radio broadcast of

Ukweli wa Mambo


Download audio file

Tafadhali, uniruhusu nikuulize, Unamwamini Yesu?  Kama unamwamini, hata kama umekosea kiasi gani, bado uko mmoja wa watoto wa Mungu.  Mlango wake uko wazi kwa ajili yako ili umgeukie.

Nawezaje kuthubutu kutamka maneno thabiti kama hayo?  Ni kwa sababu unayakuta tena na tena kwenye Neno la Mungu.  Ni kweli, watu wanatenda  mambo ya hovyo na wanapata hasara kutokana na mienendo yao, lakini Mungu yuko tayari muda wote kuwapokea pale watakapomrudia. 

Kuna wakati wana wa Israeli walitenda vibaya sana.  Mungu alitoa muhutasari wa nama walivyomkosea kwenye mistari ifuatayo: 

Malaki 3:13-15  Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema BWANA.  Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?  Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi?  Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.    Kumbe, ni hatari.  Lakini … 

Malaki 3:16,17    Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao.  Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.  Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. 

Unaona?  Walitenda vibaya.  Kwa hiyo; ilibidi wajadili hali yao wao wenyewe, halafu Mungu akasikiliza.  Ilibidi wamheshimu tena.  Na sisi pia inatubidi tumheshimu Mungu, si vingenevyo.  Umheshimu Mungu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy