Ulimi Wako na Moyo Wako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 6:45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Nataka kukuuliza? Unawatendeaje watu wengine? … Wafanyakazi wenzako, familia yako, majirani Wakati unawaangalia?
Majibu yako ya maswali hayo ni muhimu sana kwa sababu yanaonyesha yaliyomo moyoni mwako. Kwa kuwa teknolojia imepiga hatua kubwa siku hizi, ni rahisi sana kujitenga kimwili na kihisia, na watu ambao tungekuwa na mahusiano nao.
Lakini ghafla, tutajikuta gizani. Mioyo yetu itaanza kuwa migumu kwao, na kuanza kuwatengenezea mambo mabaya hatimaye, yatafurika yakitoka vinywani mwetu. Huniamini?
Luka 6:45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Yale tunayowaambia watu wengine yanadhihirisha yaliyomo mioyoni mwetu. Jinsi tunavyowatendea inaonyesha wazi tunavyowawazia. Ebu, turuhusu yafuatayo yazame katika mioyo yetu tena:
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.