... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Lakini Mimi ni Mtu Mwema

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ufunuo 1:4,5 … Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja … tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake.

Listen to the radio broadcast of

Lakini Mimi ni Mtu Mwema


Download audio file

Wakati nilipoamini na kugeuka kuwa Mkristo, nilijiuliza mara kwa mara kwa nini ilimbidi Yesu kufa kwa ajili yangu.  Kwanini alipaswa kupitia mateso yale yote?  Ukiangalia, mimi si mtu aliyefanya kosa la jinai, Kwanini ateswe?

Kuna mambo ambayo tungefanya tofauti tukiangalia nyuma.  Ni kweli kabisa kwamba tusingewaumiza wale ambao tumewaumiza kama tungekuwa na nafasi ya kurudia. Lakini Mungu ni Mungu mtakatifu, Mungu ambaye kanuni zake hazibadiliki, yeye amekamilika asilimia mia.  Pia yeye ni Mungu mwenye haki. 

Mungu huyu huyu ni Mungu wa upendo pamoja  na Haki ndivyo alivyo.  Kwa hiyo njia ya pekee aliyekuwa nayo kwa kutupenda na kutenda yaliyo haki, ilikuwa kumtuma Mwanae Yesu asulubiwe, amwage damu yake, na kutoa uhai wake aweze kulipa deni la dhambi zako na dhambi zangu. 

Ufunuo 1:4,5  … Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja … tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.  Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake. 

Kama vile Charles Spurgeon alivyoeleza: “Maadili yanaweza kukusaidia usiwekwe gerezani, lakini unahitaji damu ya Kristo kukulinda usiende Jehanamu.”  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly