Unifumbue Macho Yangu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 119:17,18 Umtendee mtumishi wako ukarimu, nipate kuishi, nami nitalitii neno lako. Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Tuna tabia ya kutafuta maajabu maishani mwetu; mambo ambayo yanaweza kutubariki. Mambo mema ambayo yangetukirimia hata kukirimia watu tunaowapenda. Lakini kuna wakati yale mema yanaweza kutupotosha.
Ni nani kati yetu hajawahi kutazamia mambo mema katika maisha yake? Labda ulitamani kuwa na nyumba kubwa zaidi, gari nzuri zaidi, au likizo ambayo ingekupumzisha kwelikweli. Au kutaka kuwa na mwenza anayefaa kufunga ndoa naye, au kama umeshaoa au kuolewa, kuwa na ndoa iliyo bora.
Kwahiyo tunaanza kutafuta mambo hayo huku tukijitahidi sana kuyapata kwa nguvu zetu zote, lakini hatimaye tunagundua kwamba hayaridhishi kama mtu alivyotazamia.
Kwa hiyo tuulize, je! Maajabu ya kweli yanapatikana wapi?
Zaburi 119:17,18 Umtendee mtumishi wako ukarimu, nipate kuishi, nami nitalitii neno lako. Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Hili ni dua zuri sana! Yaani ni jambo jema kabisa la kumwomba Mungu! Atukirimie, atusaidie kutii Neno lake, atufumbue macho yetu na kuona, kuaona nini sasa? Maajabu yatokayo kwenye sheria yake.
Acha nikwambie, tunapotanguliza dua kama hiyo kabla hatujafungua Biblia zetu, maajabu yanaanza kutokea. Roho Mtakatifu analeta hekima yake na upendo wake ndani ya maisha yetu. Anatubariki kwa kutusaidia kugundua maajabu pale pale kupitia Neno lake.
Hekima na utambuzi kuhusu sisi wenyewe kwanza, kuhusu wengine, kuhusu mahusiano tuliyo nayo, kuhusu namna tunavyotembea na Mungu na hayo yote yatatunisha maisha yetu kuliko tuwezavyo kukadiria!
Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.