Uoshwe na Roho Mtakatifu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Tito 3:5-7 Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; ili tukihesabiwe haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Ni ajabu kwamba tunafua nguo zetu wakati zinachafuka kwa kuzivaa kila siku, lakini watu wengi wanapuuza swala la kuoshwa moyoni, na penyewe panachafuliwa kwa sababu tunaishi katika ulimwengu uliooza na kujaa dhambi.
Labda nitasikika kwamba nimetaka kuvuta masikio ya watu tu, lakini ni kweli kwamba mioyo ya watu wengi imefunikwa na mawingu na mafumbo ambayo yanawaficha uharibifu wa dhambi iliyomo. Yaani mitazamo potovu, kushikilia itikadi isiyofaa, ubinafsi, tamaa ya vitu vya dunia hii. Mtu akipuuza mambo hayo kwa kweli atakuwa hatarini.
Watu hawaridhiki, hawana malengo, wanaugua kisaikolojia, mahusiano yao na watu wengine yamevunjika, maisha yamewaharibika hadi wanaonekana kuwa wazimu wanaotembea kati ya walio hai badala ya kuishi maisha tele ambayo Yesu alikuja atuletee. Sasa, ukisema ukweli, ni dalili ngapi zinaonekana katika maisha yako?
Tito 3:5-7 Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; ili tuhesabiwe haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Rafiki yangu, Yesu alikuja ili akuokoe. Alikuja ili aweze kuingia moyoni mwako aondoe mafumbo na kutibu ugonjwa wako, akuoshe, akufanye upya, akumwagie Roho Mtakatifu anayeweza kubadilisha maisha yako na kukujaza tele. Yesu alikuja kwa ajili yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.