... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Upendo Huvumilia …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 13:4,5 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hatuafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.

Listen to the radio broadcast of

Upendo Huvumilia …


Download audio file

Mimi binafsi sikubaliani na dhana ifuatayo inayosema, “Kwa nini kutamka habari kwa maneno sita wakati mtu angeweza kutumia maneno sitini?”  Lugha ya madoido pengine inaweza kushawishi watu baadhi, lakini tukiwa wazi, kupunguza maneno, ni busara.

Ndiyo maana kila siku, wakati ninaandaa ujumbe huu, baada ya kuuandika, ninachukua muda wa kutosha kupunguza maneno na kuyaweka katika lugha rahisi inayoeleweka kwa lengo la kufikia kiini cha ujumbe wake Mungu ndani ya Neno lake.  Kwa sababu kazi yangu si kuwashangaza na lugha ya madoido, bali ni kuwashirikisha habari ya upendo wenye nguvu wa Yesu Kristo kwa uwazi.

Ndiyo maana napenda Andiko hili lifuatalo.  Nguvu yake inatokana na jinsi halina makona tena linatumia maneno machache tu.

1 Wakorintho 13:4,5  Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hatafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.

Tuchunguze maneno matatu ya utangulizi.  Upendo huvumilia, hufadhili.

Kama maneno hayo matatu yangetumika kila siku na watu wa Mungu duniani kote, wewe na mimi hapa tulipo, na penginepo, ingelibadilisha kabisa ulimwengu wetu, si kweli?

Juzi nilikuwa nimebanwa na mambo mengi kabisa.  Yaani nilisumbuliwa sana halafu nikaanza kufokea watu.  Kwa hiyo nikasimama na kuvuta pumzi na kuruhusu uwezo wa Mungu utembee moyoni mwangu kupitia maneno yale matatu.  Mara moja yalibadilisha mtazamo wangu na mwenedo wangu pia.

Upendo huvumilia, hufadhili.  Yaani maneno hayo matatu ndiyo yaliyo na nguvu sana ya kubadilisha watu hata ulimwengu mzima, kuliko maneno mengine yote yangeweza kuingia moyoni mwa mtu.  Upendo huvumilia, hufadhili.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy