Ushirikishe na Wengine!
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yeremia 20:9 Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.
Ni kama inatuwia vigumu siku hizi kuongea na watu wengine kuhusu upendo wa Mungu ndani ya Yesu Kristo, kwahiyo watu wengi wameacha kumshuhudia. Lakini bado kuna kitu ndani yetu kinachotusukuma, kama unavyojua …
Sijui kama huwa unatatanishwa pale unapotaka kushirikisha wengine ambao hawajaamini habari njema ya Yesu, Labda umetishwa kwa jinsi watu wanavyokupigia kelele na kukunyamanzisha mara nyingi?
Ukweli ni kwamba, watu wa Mungu wengi wamenyamaza. Kwa hiyo, Habari Njema za Yesu zimezuiliwa; Injili ya msamaha na toba haitangazwi.
Sisemi habari za kuwa mwinjilisti au mhubiri, hapana. Si kila mtu ameitiwa hayo. Wala siongelei habari za kulazimisha watu kuikubali dini kama vile wengine wanavyofanya. Hapana. Bali ninataka kueleza namna tunavyoweza kuwaambia watu wengine kwa upole na upendo habari za Yesu kupitia maneno na matendo yetu.
Nabii katika Agano la Kale aitwaye Yeremia alitatizwa hivyo wakati anaandika maneno yafuatayo:
Yeremia 20:9 Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.
Acha Neno la Kristo liwe kama moto uwakao ndani yako, moyoni mwako, hata kwenye mifupa yako. Na mimi ninaomba uwake kiasi kwamba usiweze kabisa kujizuia ili kwa njia moja ama nyingine uweze kuwashirikisha wengine Neno la uzima.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.