... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usijaribu Peke Yako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kutoka 33:13-16 Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi?

Listen to the radio broadcast of

Usijaribu Peke Yako

Download audio file

Ni wachache sana wanaotambua mzigo mkubwa walioubeba viongozi.  Yaani, kuna siku joho la uongozi linakuwa mzigo mzito. Maamuzi makubwa ya kufanya na wakati mwingine huwa ni maamuzi yanayoashiria uzima na kifo. 

Leo tunaendelea na habari za Musa, akipambana na fursa iliyowekwa mbele yake na Mungu, ili aongoze Israeli kupitia jangwa hadi kuingia Nchi ya Ahadi. 

Watu hawa, jamani, walinung’unika, wakamkosoa, hata kumwasi Mungu kiasi kwamba Musa kwa hasira ya kutetea haki alivunja mbao zile mbili zenye Amri Kumi, kwahiyo ilibidi Musa apande mlima mara ya pili amwendee Mungu. 

Musa alijikuta amebanwa sehemu ngumu sana.  sasa alitoa dua gani mbele za Mungu? 

Kutoka 33:13-16  Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako.  Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.  Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa.  Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako?  Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? 

Muhtasari wa ombi la Musa ni upi?  Mungu, usipoenda nasi, mimi sitoki hapa!  Ni dua iliyopata kibali mbele za Mungu.  Mungu aliliheshima. 

Kwa kujikumbusha: Mungu anaweka fursa isiyowezekana mbele yako, usithubutu kuifanya peke yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy