Usijisifu kwa Ajili ya Kesho
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 27:1 Usijisifu kwa ajili ya kesho; kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.
Sijui kama ninaweza kukuuliza kuhusu mipango uliyo nayo kwa ajili ya kesho, kesho kutwa … wiki ijayo, mwezi ujao, mwaka ujao? Kuna wengine wanapanga vizuri, na wengine sio sana, lakini sisi sote tuna matumaini na matazamio ya siku zijazo, si kweli?
Maisha yanaweza kuvunjika haraka sana, lakini hata hivyo, unapoona mambo yanaenda shwari, ni rahisi kuliwazwa na kufikiri yote ni salama tu. Tunaweza kufikiri kwamba hatima yetu iko mikononi mwetu.
Mwisho wa mwaka jana mambo yalikuwa yanaenda vizuri tu. Mimi na mke wangu tulikuwa karibu kuondoka kwenda likizo kwa safari tulioiandaa mapema sana.
Lakini wiki moja kabla ya kuondoka kwenda likizo, mama yangu mzazi mwenye umri wa miaka 92 alianguka, pia mama mkwe naye akiwa na umri wa miaka 82 alipelekwa hima-hima hospitali kupasuliwa kwa dharura. Ghafla mipango yetu yote ilivurugika.
Bila shaka umeshapitia kipindi kama hicho. Yote yanaenda vizuri hadi pale mambo yanaenda kombo.
Mithali 27:1 Usijisifu kwa ajili ya kesho; kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.
Ukweli ni kwamba, hata kama wewe na mimi tunapanga mambo; na mara nyingi yanawezakutimia, hatujui kabisa yatakayozaliwa na siku moja. Hatima yetu iko mikononi mwa Mungu, si mikononi mwetu.
Ndiomaana ni muhimu sana kumsogelea, kusikiliza manong’oneza ya Roho pale tunapoandaa mipango yetu. Yeye anajua ya mbeleni na kwa kuwa anatupenda kipeo, atatuongoza kupitia Roho pale tunapopanga mambo yetu.
Bado matukio ya dharura yatatokea, lakini Mungu hawezi kushituka. Usijisifu kwa ajili ya kesho, lakini kwa unyenyekevu, kabidhi mipango yako yote mikononi mwake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.