Usinyauke Ukiwa Kwenye Mzabibu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 11:6 Haki yao wenye haki itawaokoa; bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
Ni ajabu namna dhambi;; – unajua, watu hawapendi kusikia neno hilo siku hizi –dhambi ina tabia ya kuchipuka tena maishani mwetu bila sisi kuelewa. Leo ni muda muafaka wa kujikagua na kuamka tena.
Dhambi mojawapo ya wanadamu wenye kudhuru kwa siri ni uroho, kwa sababu inaweza kuota katikati ya nia njema.
Ni kweli, sisi sote tunataka kupiga hatua mbele, ukiwa kijana unatarajia kujenga familia, kununua au kujenga nyumba, kupanda cheo kazini ili mshahara uongezeke kidogo kwa ajili ya kukidhi mahitaji … na hatimaye mtu apate uwezo wa kununua yale anayotamani.
Halafu, bila hata kufikiria, mtu anataka zaidi na zaidi, na hali hiyo itamletea mambo yasiyopendeza. Kwa baadhi, inawaingiza kwenye madeni yasiyobebeka wakivutwa kununua kwa mkopo vitu vilivyoko nje ya uwezo wao. Kwa wengine, inawapelekea kupunguza kiasi cha matoleo kwa ajili ya kazi ya Mungu (swala hilo tuliliongelea jana). Lakini kwa wengine, tamaa inasababisha waanze kutumia udanganyifu na kutafuta “njia za mkato” kwenye biashara ili waongeze mapato.
Kama nilivyosema, tamaa ni dhambi inayodhuru kwa siri kuliko zote. Sasa uko tayari kujikagua leo?
Mithali 11:6 Haki yao wenye haki itawaokoa; bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
Katika lugha ya asili ya Kiebrania, maandiko yanalinganisha uaminifu na haki, yakiwaita wasio waaminifu wasaliti. Labda inaonekana hayo maneno ni makali lakini ni sahihi kabisa.
Kwahiyo, kama uroho na udanganyifu umekuathiri siku hizi, ukikushawishi, jikague sasa hivi kabla hujapitwa na wakati. Kwa sababu …
Haki yao wenye haki itawaokoa; bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.