Usipuuze Dalili Hatarishi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 10:16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Nadhani tungekubaliana kwamba ni mtazamo mzuri kujaribu kutafuta yaliyo mema ndani ya watu wengine, tukiangalia uwezekano wao na kuchukuliana nao katika mapungufu waliyo nayo – ni jambo zuri, si kweli? Lakini kuna hatari kwa sababu mtu anaweza kuchukuliana na mtu kupita kiasi na hatimaye kujiletea madhara.
Sasa kijana anakutana na binti. Wanaanza kupendana. Anataka kumposa. Binti anakubali … hata kama kidogo katika fikra zake ana mashaka fulani kwamba pengine kuna jambo fulani lisilo sawa. Lakini si wanapendana? Binti anajua kwamba anaweza akambadilisha kijana. Wanafunga ndoa … halafu baada ya miezi sita tu, yule binti anagundua kwamba ameolewa na mume apigaye mke wake. Je! Maonyesho hayo yenye masikitiko makubwa yametokea mara ngapi duniani?
Ukweli unaosikitisha ni kwamba si kila mtu aliye kama anavyoonekana mwanzoni. Kwa hiyo, bado ni jambo zuri kutafuta yaliyo mema ndani ya watu wengine. Inadhihirisha tabia ya Mungu, sifa yake kuwa mwenye upendo. Lakini upendo huo lazima uendane na hekima pia. Yesu aliwatazamisha wanafunzi wake hivi:
Mathayo 10:16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Aliwapa tahadhari kabla ya kuwatuma kuenenda katikati ya taifa lile lenye dini, dini la watu waliokuwa milki yake Mungu, ili waweze kutangaza habari yake njema. Watu wale wangestahili kuwapokea wanafunzi kwa furaha, lakini alijua kwamba hawatafanya.
Kwa kweli, kuna utofauti mkubwa katika sentensi yake yenye tahadhari – kuwa na busara kama nyoka (maana yake, kuwaona watu jinsi walivyo kweli kweli) pamoja na kuwa wapole kama hua (wenye upendo, upole na ukarimu) – na kufanya yote kwa pamoja.
Kama vile mtu fulani alivyosema … ukipuuza dalili za hatari kwa sababu umedhamiria kuona mema tu ndani ya mtu, itakugharimu baadaye.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.