... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiwe Kama huyu Jamaa.

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 23:23,24 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.

Listen to the radio broadcast of

Usiwe Kama huyu Jamaa.


Download audio file

Kuna wakati mtu anakuwa na uhakika kwamba yeye yuko sahihi ila wengine ndio wamekosea. Ni kama kitendawili hivi. 

Hivi karibuni niliona picha ya ngazi pana sana iliyoenea milango miwili ya nyumba zilizofatana na zilikuwa zinachangia ukuta. ilikuwa majira ya baridi sana na barafu ilikuwa imeshaanguka. 

Mwenye nyumba ya upande wa kushoto alikuwa ameshafagia na kuondoa barafu iliyokuwepo upande wake tu, akaacha kama mstari usioonekana kati ya nyumba hizo mbili.  upande mmoja smafi lakini wa pili umejaa barafu. 

Sasa acha nikuulize, je! alikuwa sahihi yule bwana?  Hata kama alitumia usahihi kwa kupima vizuri, lakini Hakukosea kweli?  Chini ya  picha hiyo palikuwa pameandikwa “Usiwe kama jamaa huyu.”  Mimi binafsi nakubaliana na ushauri huo. 

Mathayo 23:23,24  Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki!  Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.  Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. 

Kuna wakati mtu anaweza kuwa sahihi asilimia 100%, lakini bado akawa amekosea asilimia 100%.  Vipi sasa kwa swala la kusimamia kanuni na kusahau ubinadamu, ustaarabu na rehema, na kusahau kuwa mwaminifu katika maadili. 

Usiwe kama jamaa yule! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy