... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Utajiri Wa Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 11:32,33 Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote. Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!

Listen to the radio broadcast of

Utajiri Wa Mungu


Download audio file

Kuna kitu cha ajabu kinatokea ndani yako pale utukufu wa Mungu unajaa moyoni mwako. Kuna mabadiliko makubwa yanayotokea maishani mwako pale unapofurahia mwanga wa upendo wake kwako.

Mara nyingi tunajikuta tunakaza mwendo, tukishughulikia maswala ya maisha, tukibanwa-banwa kwa kutafuta riziki na mahitaji mengine. Lakini hali hiyo inaweza kusababisha dhambi iongezeke na kuenea kama ugonjwa unaoathiri uzima wetu. 

Jana tulichunguza kwamba upendo wa Mungu ni mkubwa … 

Warumi 11:32  Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.    

Alikusudia kupanga mambo ili tusiweze kuishi maisha yasiyo na dhambi kwa nguvu zetu sisi wenyewe. Ametufunga sote katika uasi kwa kusudi lake ili tuweze kutambua ukubwa wa pendo lake, akituonyesha rehema zake kupitia Yesu aliyekufa ili alipe deni la dhambi zetu. 

Ebu, tafakari kwanza.  Acha ukweli huo uinue kichwa chako kwa muda huu uangalie mambo ya mbinguni. Umruhusu Mungu ajaze moyo wako na utukufu wake ukifurahia nuru ya pendo lake kwako. 

Warumi 11:33  Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu!  Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! 

Rafiki yangu, hilo ndilo lengo la Mungu kwa ajili yako; anataka ufikie kiini cha kimo chake na hekima yake kwa kumjua yeye kweli kweli.  Ndio maana Yesu alikuja.  Alikuja kwa ajili yako.  Hii ndiyo maana ya Krismasi. 

Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazichunguziki! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy