... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Unatazamia Nini?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.

Listen to the radio broadcast of

Unatazamia Nini?


Download audio file

Je!, Utaudhika nikikuuliza  swali la moja kwa moja? Je! Kuna nini moyoni mwako kipindi hiki tunakaribia Krismasi?  Una hali gani?  Unatazamia nini?  Unatumaini kupata nini?

Wakati Krismasi ya kwanza inakaribia … hawakuiita hivyo wakati ule … matazamio ya Israeli yalikuwa mbalimbali. Tangu waliporejea kwao baada ya uhamisho Babeli mwaka wa 518 kabla ya Kristo, bado walikuwa chini ya himaya ya wengine.  

Sasa, kipindi hicho Yesu anazaliwa, walitaka Mungu awaokoe na ukoloni wa kikatili wa Warumi; walitaka wapate Mwokozi, Masihi kama vile alivyowaahidi makarne mengi yaliyopita. Lakini hapo ndipo pana shida.

Mungu alikuwa amekaa kimya miaka mingi.  Alikuwa hajaongea na taifa la Israeli kupitia nabii kwa karne nne.  Ilikuaje?  hivi Masihi atakuja kweli?  Si walikuwa teule wa Mungu?  Lakini Mungu alikuwa na mpango wake … ila mpango wake ilikuwa tofauti na mipango yao. 

Mika 5:2  Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele. 

Mpango wa Mungu ilikuwa Mwokozi azaliwe bila kutazamiwa sehemu isiyojulikana.  Hata kama alinyamaza miaka mingi sana, Simba alikuwa anajiandaa kuunguruma … ila angeingia ulimwenguni kama mwana kondoo, kama mtoto katika hori la ng’ombe. 

Hawakutazamia hilo.  Lakini mtoto yule alikuwa mkuu kuliko walivyofikiria  Mungu alimtuma Yesu, Mwokozi wa ulimwengu aje kwa ajili yao.  Mungu alimtuma Yesu, Mwokozi ulimwengu kwa ajili yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo