... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Utamjua kwa Kumtii

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 14:22,23 Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

Listen to the radio broadcast of

Utamjua kwa Kumtii


Download audio file

Lazima mtu ajihadhari na watu wanaojidai kwamba wao wamepata kufunuliwa jambo ambalo wengine hawakulipokea.  Lakini sisi Wakristo, ndivyo tunavyodai; kwamba tumepewa ufunuo wa Mungu mwenyewe usio wa kawaida.

Wakati Yesu alikuwa anaelekea kwenye msalaba ambapo angelipa deni la dhambi za ulimwengu, za kwako na za kwangu ili tupate kusamehewa, ili tuweze kuishi milele mbele zake, Yesu alisema jambo lisiloeleweka; yaani jambo lenye changamoto; jambo ambalo lapaswa kufafanuliwa vizuri zaidi.  Alitamka hivi: 

Yohana 14:18,19  Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.  Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 

Ina maana, ninyi nitawafunulia habari inayonihusu ambayo wengine hawataipata.  Lazima neno hilo lifafanuliwe.  Kwa hiyo …

Yohana 14:22  Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?   

Swali zuri.  Zuri sana. 

Yohana 14:23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.  

Mwisho wa siku, je!  Tunawezaje kumjua Yesu?  Tunawezaje kumfahamu kila mmoja wetu?  Kwa kumpenda na kumtii.  Ni nafsi yenye utii ambayo ingefunuliwa Yesu; pia mtu mwenye moyo huo ndiye Baba yake na Yesu mwenyewe wangeweza kuja kufanya makao ndani yake kwa njia ya Roho Mtakatifu. 

Usipuuze umuhimu wa utii na uwezo wake katika uhusiano wako na Yesu.  Usiupuuze!  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy