Uwe na Mipango
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 2:10-12 Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yatakupendeza nafsi yako; busara itakulinda; ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, na watu wanenao yaliyopotoka.
Inabidi tumtegemee Mungu. Sote tunafahamu kwamba inatupasa kumtegemea Mungu. Kama umewahi kusoma Biblia shaka bila shaka utakuwa umeshasikia Mungu akuirudia-rudia, akisema, Unitegemee. Lakini kumtegemea Mungu kusimfanye mtu kuwa mzembe.
Katika miaka hii isiyo michache nikiwa kwenye huduma, nimewaajari watu wengi. Baadhi walikuwa wafanyakazi wazuri sana, lakini wengine walikuwa wavivu. “Si huduma ya Kikristo? Si inahusu upendo? Kwahiyo sina haja ya kutumika kwa nguvu.”
Sasa nimetengeneza hotuba fupi kwa ajili ya wafanyakazi wapya. Ninawaambia kwamba ninatazamia watafanya makosa wote. Hakuna mtu asiyefanya kosa. Hii haina shida. Baada ya kukosea, mtu anapaswa kusimama tena, akubali kosa lake bila kulaumu wengine, ajifunze, aendelee na kazi, basi. Lakini … Kuna mambo matatu ambayo siwezi kuyavumilia hata kidogo – nacho ni mtazamo potovu, udanganyifu na uvivu.
Siku hizi tatizo la uvivu limesambaa sana kwa Wakristo. “Kwa kuwa ninamtegemea Mungu, atashughulika yeye mwenyewe, sina haja ya kujitahidi sana. Sina sababu ya kuandaa mipango ya baadaye, si kazi yake yeye?” Jamani, inakuwa hivi kweli?
Mithali 2:10-12 Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yatakupendeza nafsi yako; busara itakulinda; ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, na watu wanenao yaliyopotoka.
Ukiishi kwa bidii na maadili, utaongezwa hekima. Utajifunza mengi na yatakuletea furaha. Lakini angalia maneno yafuatayo: kuwa na mipango kutakulinda na ufahamu utakuhifadhi.
Mungu anatazamia kwamba, tukiwa chini ya mkono wake basi tuwe na mipango. Ni Kwanini? Ni kwa sababu busara, mipango pamoja na ufahamu vitatulinda, Pia, vitatulinda na wenye mipango mibaya juu yetu.
Kwahiyo … usiwe mvivu. Panga mapema sana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.