Uwezo Ndio Uthibitisho
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 2:3-5 Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. Na neno langu la kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
Sijui kama umeshaona jinsi ilivyo vigumu kuachana na tabia mbaya hata moja Kuacha kuvuta sigara, kuthibiti hasira zako za karibu, kukabiliana na mtazamo hasi unaoleta sumu moyoni kwa kuzungusha fikra kichwani kwamba hufai. Haijalishi ni tabia gani mbaya, hazitaki kukuacha.
Wiki hii tunayoimalizia tumesimulia habari za ukubwa wa upendo wa Mungu kwetu pale alipomtuma Yesu kufa Msalabani ili alipe deni la dhambi zako na dhambi zangu. Kwa watu wengi alichofanya Yesu hakieleweki, ni upuuzi tu.
Hata hivyo, hakuna upendo mkubwa katika historia ya binadamu kuliko ule ulioonekana pale Mwana wa Mungu alipotundikwa Msalabani bila kuwa na hatia ili alipe deni ambalo wewe na mimi tusingeweza kulilipa.
Lakini thibitisho liko wapi? Tutawezaje kujua kwamba habari hiyo ni ya kweli?, Tutawezaje kujua kama Ukristo kwa ujumla unafanya kazi kweli kweli? Huu ndio uthibitisho ambao Paulo aliwaandikia kanisa lililokuwa Korintho kwenye karne ya kwanza.
1 Wakorintho 2:3-5 Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. Na neno langu la kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
Je!, Unatafuta uthibitisho? Thibitisho ni katika uwezo. Si ndani ya mahubiri mazuri au maneno matupu. Si kwa sababu mimi ninathibitisha wala kwa sababu Biblia inathibitisha tu. Bali ni kwasababu mtu anapzweka imani yake ndani ya Yesu, Bwana anaachilia uwezo wake mkubwa kumsaidia kuishi katika ushindi dhidi ya tabia zake mbaya – ili awekwe huru na dhambi zake.
Kwa ufupi tu, Ukristo unafanya kazi kweli kweli. Uthibitisho ni katika uwezo wake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.