Uwezo wa Tabia Njema
Add to FavouritesYakobo 1:22-25 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Jambo lenye nguvu sana maishani mwetu – nguvu iletayo mema au mabaya – ni tabia tunazojizoesha (kwa wema) au tabia mbaya zinazotuangusha (ndani ya uovu). Najiuliza, Tabia zako wewe zikoje? Ni njema kiasi gani?
Mimi nikiwa mtu anayechukia sana kufanya mazoezi ya kimwili, nilikuwa ninawasikiliza wataalamu wakisema, “Lazima ufanye mazoezi hasa unapozidi kuzeheka,” lakini nikapuuza. Hadi siku moja mwanzo wa mwaka huu, nilisadikishwa moyoni mwangu kwamba nisipoanza kufanya mazoezi, misuri yangu hata mifupa yangu itaendelea kuchakaa haraka … hali ambayo itaniathiri mapema katika uzee wangu.
Kwa hiyo, kila asubuhi kasoro Jumapili, nikiamka tu, nafanya mazoezi kwa mikono na miguu, halafu mara tatu kwa wiki ninakimbia ili mapigo ya moyo wangu yapande kwa muda. Na kweli najisikia vizuri sana kutokana na mazoezi hayo. Lakini kusikiliza wataalamu haikuleta mabadiliko mazuri, bali ni utekelezaji na kufanya mazoezi ile niwe na tabia ya kuyapenda. Hivyo ndivyo inavyotakiwa hata kwa habari inayofuata …
Yakobo 1:22-25 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Kwa hiyo … usikae bure. Simama, tembea.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.