... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kustahilimi si Kukaa tu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 1:12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Listen to the radio broadcast of

Kustahilimi si Kukaa tu


Download audio file

Majaribu ya kutenda mabaya huwa yanatujia kila siku. Na tunaweza kushindwa kama wengi wanavyoshindwa au tunaweza kustahimili na kusimama imara.  Sasa kwako wewe itakuwaje?

Kama ilivyo kwenye jambo lolote maishani, tunaweza kukabiliana na majaribu kwa kukaa tu au kuwahi na kujihami mapema. Watu wanakaa tu na kusubiri kitakachokuja huwa wanapelekwa na mkondo. Mara nyingi watu kama hawa wanawalaumu watu wengine kwa matatizo waliyo nayo. Lakini ni kama wanajifanya wenyewe kuwa shabaha ya adui, Ibilisi anafurahia kuwavizia tena na tena. 

Kwahiyo, majaribu yakikujia katika maisha yako, Wewe  huwa unakaa-kaa tu na kuyasubiri au huwa unakuwa chapu kujihami? 

Yakobo 1:12  Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. 

Changamoto iliyopo katika majaribu ni kusimama imara na kuwa mwaminifu na hivyo kuthibitisha imani yako. Imani bila matendo imekufa, si kweli?  Matendo yetu mema ni uthibitisho kwamba imani yetu ni ya kweli. Ni mada inyoonekana ndani ya Biblia tangu mwanzo hadi mwisho. 

Wewe unafahamu mambo yanayokuwa jaribu kwako. Pia unafahamu madhaifu yako.  Kwa hiyo inabidi ujiandae mapema ukisubiri jaribu likujie, sababu halina budi kuja.  Je! Umejipangaje pale mtu anapokukasirisha? Je!, Una mpango gani pale unapojaribiwa udanganye?  Je!, Una mpango gani?  Hmm? 

Ni akina nani wanaweza kwenda vitani wakiwa na uhakika kwamba wanaenda kuvamiwa na adui bila kuwa na mpango wowote wa namna watakavyojihami na kuwashinda?  Yaani wangekuwa wamepumbazika sana, si kweli?! 

Kwahiyo, uwe na mpango.  Kwa sababu bila shaka majaribu yanakuja.  Kustahimili si kukaa-kaa tu, bali ni kujiandaa mapema. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.