Uwezo wa Uzima
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 5:20,21 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu. Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.
Hakuna awezaye kukana miujiza ya ajabu Yesu aliyofanya. Alifanya viwete watembee, vipofu waone, Lazaro kufufuka kutoka kaburini. Lakini miujiza hiyo ilikuwa na maana gani? Inatusaidia nini leo?
Siku hizi chache tumesimulia habari ya Yesu kutenda muujiza mkubwa wa kumwezesha kiwete aliyekuwa analala chini kuamka na kuanza kutembea. Ebu fikiria ingekuwaje kama ungeushuhudia. Ebu fikiria kama wewe ungekuwa kiwete yule aliyetendewa ajabu lile.
Halafu baada ya miaka elfu mbili bado tunasoma na kuongea habari ya miujiza yake Yesu. Kwa nini? Miujiza hiyo inaashiria nini? Ina maana gani kwetu sisi leo? Ebu sikiliza jibu alilitoa Yesu mwenyewe:
Yohana 5:20,21 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu. Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.
Ina maana kwamba wewe na mimi tujue ya kuwa Yesu ana uwezo – kwamba yeye mwenyewe ndiye uwezo – kutupa uzima, uzima wa kweli, uzima wa milele! Kabla watu hawajaweka imani yao ndani ya Yesu, ni wafu katika dhambi zao, ni wafu wanaotembea juu ya nchi, ni wafu wenye uharibifu wa milele.
Lakini ndipo Yesu anaingia katika maisha ya mtu na Roho wake anampa uwezo na nia ya kumwamini. Kumwamini kwa ajili ya nini? Kwa ajili ya uzima! Uzima tele aliyeahidi kumpa hapa duniani; uzima wa milele aliompa kupitia imani kwa kufufuka kutoka wafu.
Mimi ndimi njia na kweli … na uzima.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.