Wivu Wa Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Kutoka 20:2,3,5 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi … Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao.
Acha nikuulize, je! ni kipi ulicho nacho ambacho kingekuwia viguma sana kuachana nacho kama Mungu angekuomba ukiache? Ni mali gani au cheo gani au tabia gani … ingekuwia vigumu kuiacha?
Kwangu mimi ni teknolojia. Tangu zamani napendezwa sana na mitambo ya teknolojia – nilikuwa na kampuni ya teknolojia karibia kwa takribani miaka ishirini. Ninapendela kufanya vyombo vyangu vyote – saa, simu, komputa ndogo na kubwa – vyote vifanya kazi sambamba, napenda niboreshe uwezo wa utendaji wa kila chombo.
Kama Mungu angeniomba niviache vyote na kutumia karamu na kartasi tu, kwa kweli ingeniwia vigumu mno. Sasa ngoja nikuulize tena … ni kitu gani kingekuwia vigumu kukiacha?
Kuna sababu yakukuuliza hivyo. Sisi tunaokiri kwamba tumemwamini Yesu, sisi tunaodai kwamba tu wanafunzi wake, inabidi tuchunguze vizuri kila kitu ambacho tunaweza kukitanguliza kuliko Mungu mwenyewe.
Kutoka 20:2,3,5 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi … Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao.
Kwanini Mungu ni Mungu mwenye wivu? Ni kwasababu anatupenda kuliko tuwezavyo kueleza, kwahiyo alimtuma Mwanae Yesu kufa kwa ajili yetu, ili tuweze kusamehewa dhambi zetu na kujua namna anavyotupenda.
Hataki tupotoshwe na lagha za dunia hii au Shetani,
Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.