... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kiburi Kinaharibu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 2:3,4 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Listen to the radio broadcast of

Kiburi Kinaharibu


Download audio file

Je!  Unapenda kuishi au kufanya kazi na mtu mwenye kiburi?  Au labda umezungukwa na wenye kiburi zaidi?  Haipendezi kwa kweli.

Bila shaka, mtazamo unaoleta uharibifu kuliko vyote ni mtazamo wa majivuno kwa sababu mwenye kiburi anajali mambo yake tu.  Anafikiri yeye ndiyo kitovu cha viumbe vyote – anajali hisia zake tu, matamanio yake, jinsi wengine wanavyomwangalia yeye, basi.

Matokeo ni kwamba amekuwa kipofu kwa wengine, asione wala kujali mahitaji yao, hisia zao, uwezo wao na mchango walio nao.  Hasiti kukukanyaga ili afikie anapolenga yeye.  Atakupuuza, atakusaliti, atakufitinisha ili ajiinue machoni pake mwenyewe hata machoni pa wengine.

Ndiyo maana Mungu anawapinga wenye kiburi akiwapa wanyenyekevu neema.  Ndiyo maana anatwambia wewe na mimi yafuatayo kuhusu kiburi chetu:

Wafilipi 2:3,4  Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.  Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Ni ushauri wenye busara kabisa.  Lazima tudhibiti majivuno yetu kama tunataka kumfuata Yesu ambaye hata kama alikuwa Mwana wa Mungu, alijishusha hadi kifo; tena kifo kibaya cha msalaba.

Lakini pia, ni ushauri unaotulinda kwa kutuonya kuwa na tahadhari tukichagua marafiki.  Kama vile alivyosema mtu fulani, uwe ange ni wepi unaowaruhusu kupanda chombo chako, kwa sababu kuna watu wengine wanaweza kuzamisha boti nzima kama hawawezi kugeuka kuwa kepteni.

Je!  Ni wepi unaowaruhusa kukuzunguka?  Je!  Wanastahili kweli kusafiri ndani ya boti yako?

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.