... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kusubiri Mafanikio Mapya

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wagalatia 6:9,10 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

Listen to the radio broadcast of

Kusubiri Mafanikio Mapya


Download audio file

Sio rahisi kuvuta subira hadi Mungu akupe mafanikio mapya katika maisha yako, popote pale panapohitajika mabadiliko, ni vigumu mno.  Halafu, kadiri hitaji lako linalokuwa kubwa, ndipo unakuta matumaini yako kwake hua yanapanda na kushuka.  Sijui kama umewahi kuona hilo?

Pengine haja yako ni katika swala la uchumi au afya yako au magonjwa ya mpendwa fulani.  Pengine inahusu mahusiano magumu ambayo yanakuathiri moyoni.  Kwa vyo vyote, wakati mtu anajikuta katika hali hiyo, inaumiza sana wakati anaendelea kusubiri akijiuliza … Je!  Mungu atanionekania?  Je!  Atatenda kulingana na hitaji langu? 

Umemwomba Mungu alete mafanikio mapya.  Wakati ulisoma habari ya uaminifu wake katika Maandiko, kwa kweli amani yake ilifunika moyo wako.  Uliona kwamba yeye ni wa kutegemea.  Lakini baadaye, ulikosa usingizi usiku, ukijigeuza-geuza kwa chomwa na hofu moyoni.  

Hatimaye ulisongwa na mawazo mengi.  Ulijikuta unaelekea hatarini na hajakuonekania.  Ulifanyaje wakati uliendelea kusubiri jibu lake? 

Wagalatia 6:9,10  Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.  Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio. 

Ina maana, ukimsubiri Mungu akuonekanie, katikati ya kipindi kile kigumu, endelea kufanya kazi na kuwa kama mhudumu hotelini, akisubiri kupokea mahitaji ya wateja.  Hudumia watu na mengine umwachie Mungu. 

Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.