... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kweli Kudhihirika

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 14:8-11 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

Listen to the radio broadcast of

Kweli Kudhihirika

Download audio file

Kweli ni mada inayojadiliwa sana kipindi hiki kilichoachana na Ukristo kabisa, mahali ambapo kila mtu anatetea “kweli” yake ili apate ushindi, aonekana kama yeye ndiye “topu”.

Katikati ya kelele ya mashindano hayo ya kujua hiyo “kweli” iko wapi, bado Mungu anataka kutwambia ukweli unaodumu kwamba alimtuma Mwanae ili atuokoe.  Ana hamu sana tukutane na upendo wake, neema yake, na rehema yake ndani ya Yesu.  Hii ndiyo kweli kabisa.  Sasa, tuulize, je!  Mungu aliamua kudhihirisha kweli yake kwa njia gani? 

Yohana 14:8-11  Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.  Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo?  Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?  Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu?  Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.  Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la!  Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 

Mungu alitwambia kweli yake kwa kujivika mwili.  Alijidhihirisha ndani ya maisha yetu yaliyochafuliwa kwa njia ya uhusiano. kama vile Yesu alivyoweza kutembea kwa miguu akiwa na wanafunzi wake wakipitia njia za mavumbi huko Israeli karne ile ya kwanza. 

Rafiki yangu, Yesu ndiye kweli.  Kadiri mtu anazidi kumjua na kumwamini na kukaa naye … ndipo Yesu atazidi kubadilisha maisha yake.  Kwa kuwa, aliyemwona Yesu, tayari ameishamwona na Baba.  Hii ndiyo kweli. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo